Swahili / Swahili

Majibu ya maswali yanayohusu lugha ya nyumbani na mafunzo sambamba

Nani anaweza kupata mafunzo ya lugha ya nyumbani?
Mtoto ambao ana lugha nyengine ya nyumbani zaidi ya kiswidi na pia ana angalau mmoja katika wazazi wake ambao anaongea ingine lugha nyumbani. Ni lazima mtoto awe na maarifa ya msingi kwa  lugha hiyo, pia awe na umri wa myaka sahihi unayohitajika kuanza mafunzo ya lugha hiyo. Mtoto ambaye ametimiza mahitaji hayo hua ana haki za kupata mafunzo ya lugha ya nyumbani.

Nifanye nini kama nataka mtoto wangu apate mafunzo ya lugha ya nyumbani?
Kazi yote hufanyika huko Chekechea ya mtoto wako. Unawambia kwamba unataka mtoto wako aanze kupata mafunzo ya lugha ya nyumbani. Kisha mkurugenzi wa chekechea anaandikia ofisi ambayo ni wajibu kwa kufundisha lugha za nyumbani hapa kwenye  manispaa ya Uppsala na baadae mtoto kuandikwa katika orodha za ofisi hiyo. Mwalimu wa lugha ya mtoto anajulishwa na ofisi yenyewe kuhusu mtoto huyo. Kazi ifuatayo ni yeye mwalimu kwenda kwenye chekechea ya mtoto ili apate kujuwa ni msaada gani ambao mtoto wako anahitaji.

Kwa nini ni muhimu mtoto ajuwe lugha ya nyumbani?
Kujuwa lugha ya nyumbani inampa mtoto nafasi ya muungano na uhusiano zaidi na familia yake pia na ndugu zake; isitoshe inamsaidia mtoto kujuwa vizuri kiswidi.
Kuweza kuwasiliana katika lugha ya nyumbani na pia angalau moja katika  lugha za kigeni ni viwili katika vitu vinane kuhusu ujuzi muhimu vinavyotajwa na Jumuiya ya ulaya ambavyo mraia yeyote wa jumuiya hiyo anastaili kuwa anaweza.
Ufahamu wa mambo ya utamaduni na kujuwa lugha ni vitu ambavyo huenda pamoja.

Kwenye umri wa myaka mingapi mtoto ataweza kupata mafunzo ya lugha ya nyumbani?
Mtoto anaweza kupata msada huyo kutoka kipindi kile anaanza chekechea kutokana na fursa zilivyo.

Wapi mtoto wangu atapatia mafunzo ya lugha ya nyumbani?
Mwalimu wa lugha anamkutana mtoto kwenye chekechea yake au ingine ya karibu ya nyumbani. Kuna  zingine lugha hutolewa mafunzo mahali ambako pamechaguliwa kuwa ni katikati watoto wataweza kukutania na mwalimu.

Ni aje mwalimu wa lugha ya nyumbani anafanya kazi?
Tunafanya kama wangine walimu wa chekechea. Tunatumiya mitaala na nyaraka za sera tunavofundisha lugha.
Tuko katika makundi ya watoto na tunashirikia katika shughuli za chekechea. Mbinu za mambo ya utamaduni zinasaidia watoto kuelewa utofauti uko kati ya watu  na pia  zinawapa zana za kuelewa dunia ilivo.

Nani anasimamia gharama za kazi hizo?
Manispaa ya Uppsala (Uppsala kommun)

Mtoto wangu anaweza kujifunza lugha nyingi kwa wakati mmoja?
Ni kweli mtoto anaweza kujifunza lugha nyingi.

Ni aje nimsaidie mtoto wangu kujua vizuri lugha ya nyumbani?
Ongea na tumia lugha ya nyumbani na mtoto wako. Unavoongea na mtoto, hakikisha kua umetumia kiwango cha juu kidogo ya maarifa yake kusudi lugha yake isonge mbele.
Tumia lugha rasmi unavoongea na mtoto na pia utumie maneno ya kuelezea, kwa mfano `` Unaweza kutia kile kitabu chewupe juu ya ile meza nyekundu `` badala ya kusema `` Kitie pale ”
Kusoma vitabu ni muhimu sana, na unaweza kuvipata kwenye maktaba.
Kukutana na watu/watoto wangine ambao wanaongea iyo lugha yako ya nyumbani inasaidia.

Tunaongea lugha ya nyumbani, si ingelikua bora kuongeya kiswidi kwa sababu kinaongewa na watu wengi?
Ni vizuri kutumia kila siku lugha ya nyumbani mnavozungumza nyumbani. Ni Lugha ambao unaelewa na unaongea vizuri, na isitoshe ni lugha ya matumizi unavoeleza hisiya zako na maoni yako ukitumia vivuli tofauti. Kwa hiyo mtoto atasikiliza lugha nzuri na tena kamili ambao ataweza naye kuitumia.

Uppdaterad: